IQNA

Jeshi la Misri lauhujumu msikiti kwa mizinga huko Sinai

23:56 - July 24, 2016
Habari ID: 3470471
Jeshi la Misri limeushambulia kwa misingi msikiti mmoja katika Rasi ya Sinai, na kuharibu sehemu za msikiti huo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, tovuti ya arabi21.com imeripoti kuwa, Msikiti wa Abu Rafaei , katika mji wa Mabedoui wa Sheikh Zuweid katika jimbo la Sinai Kaskazini ulishambuliwa na jeshi Alkhamisi usiku.

Katika hujuma hiyo nakala za Qur’ani ziliharibiwa na msikiti pia ukapata hasar aya uharibufu wa maeneo ya jengo lake.

Picha za uharibifu wa msikiti huo zimesdambazwa katika intaenti kuanzai siku ya Jumapili.

Hadi sasa haijabainika ni kwa nini Jeshi la Misri liliamua kutekeleza hujuma dhidi ya eneo hilo la ibada.

Kwa muda wa karibu miaka mitano sasa Jeshi la Misri limekuwa likijaribu kutuliza uasi mkubwa unaoendelea kote katika Rasi ya Sinai. Mapigano katika eneo hilo yamepelekea mamia ya watu kuuawa wakiwemo wanajeshi wa Misri na pia wafuasi wa makundin ya magaidi wakufurishaji.

Mnamo Oktoba 2014 hali ya hatari ilitangazwa kote katika Rasi ya Sinai baada ya magaidi kutekeleza hujuma iliyopielekea wanajeshi 33 kuuawa.

3517216

captcha