IQNA

Nakala 80,000 za Qur'ani zasambazwa Tanzania

20:23 - October 31, 2016
1
Habari ID: 3470645
IQNA-Shirika moja la misaada la Qatar limesambaza nakala 80,000 za Qur'ani miongoni mwa Waislamu nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Qur'ani la Kimataifa, IQNA, Shirika la Misaada la Sheikh Thani Ibn Abdullah, RAF, limesambaza nakala hizo za Qur'ani katika mradi ujulikanao kama Tibyan.

Taarifa zinasema taasisi, vituo na mashirika kadhaa ya Kiislamu katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki yamepokea nakala hizo za Qur'ani katika hafla iliyofanyika hivi karibuni mjini Dar es Salaam.

Maafisa wa RAF wanasema lengo lao ni kueneza mafundisho ya Qur'ani na kulea kizazi cha vijana Waislamu waliohifadhi Qur'ani Tukufu.

Shirika hilo limesema hadi sasa limesambaza nakala milioni 1.2 za Qur'ani zenye tarjama kwa lugha sita za Kiafrika, Kiasia na Ulaya.

Kati ya nchi ambazo hadi sasa zimepokea nakala za Qur'ani kutoka RAF ni pamoja na Uganda, Gambia, Mauritania, Nigeria, Sierra Leone, Ufilipino, Niger, Mali na Kenya.

3542078

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Adam Kassim Ahmadi
0
0
Assalaam alaykum. Nashmkuru Allah na ninatumai kuwa malengo ya taasisi you ya IQNA yatafikiwa na Malipo makubwa yatapatikana. Ila, Sisi pia ni miongoni mwa Watu wanao hitaji misaada hii ya Quran. Mimi ni Ustadhi na nina madrasa ya kuhifadhisha Quran. Tupo Kata ya Kazuramimba, Wilaya ya Uvinza, Mkoa wa Kigoma. Madrasa inaitwa MADRASAT FIYSABIYLILLAHI ISLAMIYYA.
Kwa Mawasiliano:- 0762146664 au 0614601110.
Ahsantum.
captcha