IQNA

Kwa munasaba wa kutekwa Pango la Ujasusi (Ubalozi wa Marekani)

Nara za 'Mauti kwa Marekani' Zarindima Iran+PICHA

15:48 - November 03, 2016
Habari ID: 3470649
IQNA-Wananchi wa matabaka mbali mbali Iran kuonyesha dhidi ya madola ya Kiistikbari hasa Marekani huku wakitoa nara za 'Mauti kwa Marekani'.
Nara za 'Mauti kwa Marekani' Zarindima Iran+PICHA

Wananchi wa matabaka mbali mbali Iran wakiwemo wanachuo na wanafunzi leo Tarehe 13 Aban inayosadifiana na Novemba 3 wameandamana mjini Tehran na kote katika Iran ya Kiislamu na kuonyesha kuwepo mpana ujumbe wa kweli na wenye taathira wa Mapinduzi ya Kiislamu dhidi ya madola ya Kiistikbari hasa Marekani.


Maandamano ya Siku ya Kitaifa ya Kupambana na Uistikbari wa Kimataifa yamefanyika Alhamisi na kuonyesha umoja baina ya kizazi cha zamani na kizazi kipya na wote kwa sauti moja wameonyesha kuchukizwa kwa na uistikbari wa kimataifa kwa kutoa nara za nara za 'Mauti kwa Marekani' na 'Mauti kwa Israel'.

Maandamano hayo yameonysha kuwa,  watu wa Iran, sawa na miaka 37 iliyopita, wanafahamu kikamilifu kuhusu njama za Marekani dhidi ya Iran na kwamba hawaliamini dola  hilo la kibeberu. Tarehe 4 Novemba mwaka 1979, wanafunzi wa Iran katika kulalamikia njama za Marekani dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran walivamia na kuzingira 'Pango la Ujasusi' (Ubalozi wa Marekani) mjini Tehran kwa lengo la kuzuia dola hilo la kibeberu kufikia malengo yake haramu dhidi ya mapinduzi machanga yaliyokuwa yamefikia ushindi Februari mwaka huo.

Nyaraka zilizofichuliwa katika Pango la Ujasusi zilithibitisha kuwepo uadui na njama kubwa sana za Marekani dhidi ya taifa la Iran.

Njama hizo zinaendelea hadi leo kwa njia mbali mbali na hata baada  vijana wanamapinduzi na wabunifu kuteka Pango la Ujasusi, lakini adui angali anaendeleza njama zake. Kwa msingi huo kizazi cha vijana wanamapinduzi hivi leo kina ufahamu wa kina zaidi kuhusu uadui wa Marekani dhidi ya Iran na hivyo vijana hao wamechukua hatua za kuzuia njama zaidi za dola hilo la kibeberu.

Ubunifu wa vijana wa Iran katika kuteka Pango wa Ujasusi mjini Tehran ulikuwa na taathira kubwa kiasi cha Imam Khomeini MA kuutaja ubunifu kuwa kuwa, 'Mapinduzi ya Pili'.

Kauli hii ya  Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilitokana na kina cha njama na ukhabithi wa Marekani wakati wa Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na baada ya hapo. Punde baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, dola la kiistikbari la Marekani lilianza kutekeleza njama dhidi ya haya mapinduzi ya watu wa Iran. Lakini kutokana na uangalifu wa watu wa Iran, njama hizo zilisambaratishwa.

Kama alivyosema Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, kutekwa Pango la Ujasusi kulikuwa ni jibu muafaka la wananchi dhidi ya uadui wa dola la Marekani linalojitakia makuu ambalo kwa miaka mingi lilikuwa likipora utajiri wa Iran lakini mikono yake hiyo  ilikatwa kufuatia ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Kwa maneneo mengine ni kuwa, kutekwa Pango la Ujasusi la Marekani Tehran kulikuwa ni mwisho wa satwa yake nchini Iran. Jambo hilo linaonyesha madola makubwa kama Marekani yatafeli katika njama zao dhidi ya Iran. Kuendelea uadui wa serikali mbali mbali za Marekani dhidi ya Iran kumetokana na kuendelea moyo wa chuki dhidi ya Marekani miongoni mwa wananchi wanamapinduzi Iran.Nara za 'Mauti kwa Marekani' Zarindima Iran+PICHA

Kusimama kidete Imam Khomeini MA mbele ya Marekani na pia kauli yake aliposema "Pegeni Kelele Muwezavyo Dhidi ya Marekani" ni ishara ya ufahamu wake wa kina kuhusu uadui wa Marekani dhidi  ya Iran na hilo limethibitika katika historia.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei amesema kuvunja Marekani ahadi zake katika mapatano ya nyuklia ni misdaki ya wazi ya kuendele auadui wake dhidi ya Iran. Amsisitiza kuwa, njia muhimu zaidi ya kustawi nchi si katika kufanya mazungumzo au kujikurubisha na Marekani bali ni kutegemea uwezo wa vijana ndani ya nchi na kuwa macho mbele ya sera hasimu za Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika taarifa ya mwisho wa maandamano ya Tarehe 13 Aban Alhamisi hii, washiriki wamesema hatu ya wananchi wa Iran kupinga dhulma na kupinga uistikbari imetokana na misingi ya Qur'ani Tukufu na mtazamo wa kimantiki. Aidha washiriki wamesema wataendelea na mkono huo kwa kufuata miongozo ya Imam Khomeini MA na pia kwa kutii amri zenye hekima za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mbele ya uistikbari wa kimataifa.

Historia ya Aban 13 (Novemba 14)

Katika utamaduni wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran Aban 13 inajulikana kama Siku ya Taifa ya Kupambana na Uistikbari. Mnamo tarehe 4 Novemba ya mwaka 1964, 1978 na 1979 yalijiri matukio matatu muhimu katika historia ya Iran. Nukta ya pamoja katika matukio matatu hayo ni mapambano ya wananchi wa Iran ya kupigania kujitawala, uhuru na kujitoa kwenye makucha ya satua na ubeberu wa Marekani. Katika tukio la kwanza la mwaka 1964 Imam Khomeini alilazimishwa kuondoka nchini na kupelekwa uhamishoni Uturuki na hatimaye Iraq kwa sababu ya upinzani wake dhidi ya misimamo ya utawala wa Kifalme ya kujidhalilisha na kujidunisha mbele ya Marekani. Katika tukio la pili la tarehe 4 Novemba mwaka 1978 vikosi vya utawala kibaraka wa Shah viliwaua kwa kuwapiga risasi wanafunzi kadhaa mbele ya chuo kikuu cha Tehran. Na ama katika tukio la tatu lililojiri katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja baada ya Mapinduzi ya Kiislamu wanachuo wanaofuata miongozo ya Imam Khomeini waliuvamia na kuuteka ubalozi wa Marekani hapa Tehran na kukomesha ubeberu wa moja kwa moja na usio wa moja kwa moja wa Washington katika nchi hii.Nara za 'Mauti kwa Marekani' Zarindima Iran+PICHA
Nara za 'Mauti kwa Marekani' Zarindima Iran+PICHANara za 'Mauti kwa Marekani' Zarindima Iran+PICHANara za 'Mauti kwa Marekani' Zarindima Iran+PICHA

Nara za 'Mauti kwa Marekani' Zarindima Iran+PICHA
Nara za 'Mauti kwa Marekani' Zarindima Iran+PICHA
Nara za 'Mauti kwa Marekani' Zarindima Iran+PICHA
Nara za 'Mauti kwa Marekani' Zarindima Iran+PICHA
Nara za 'Mauti kwa Marekani' Zarindima Iran+PICHA
Nara za 'Mauti kwa Marekani' Zarindima Iran+PICHA
3543140


captcha