IQNA

Wapalestina waandamana kupinga marufuku ya Adhana

18:12 - March 12, 2017
Habari ID: 3470890
IQNA-Maelfu ya Wapalestina wameandamana kupinga sheria ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kupiga marufuku adhana katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu.

Katika maandamano ya Jumamosi, watu zaidi ay 3,000 walikusanyika katika mji wa Kabul wenye wakaazi waarabu kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.

Washiriki waliapa kuendeleza kuadhini misikitini n ahata kuongeza kiwango cha sauti kama ishara ya kupinga agizo hilola Israel.

Kwingineko, idadi kubwa ya Wapalestina wameweka vipaza sauti vya adhana katika paa za nyumba zao kama njia ya kuonyesha upinzani wao kwa sheria ya Bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel kupiga marufuku ya adhana katika mji wa Quds na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Duru za habari zinaarifu kuwa, Wapalestina wameweka vipaza sauti vya adhana katika paa za nyumba zao huku wakisisitiza kuwa, sauti ya adhana kamwe haitazimika katika mji wa Quds.

Wakati huo huo, Farhan Haq, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani hatua hiyo ya Israel kupiga marufuku adhana. Amesema Israel inapaswa kuheshimu haki za kidini za Wapalestina.

Siku ya Jumatano,Bunge la Utawala wa Kizayuni wa Israel, Knesset, lilipitisha rasimu ya sheria ya kupiga marufuku adhana katika misikiti yote iliyopo katika mji mtakatifu wa Quds unaokaliwa kwa mabavu.

Kwa muda mrefu sasa utawala wa Kizayuni wa Israel na walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakitekeleza njama ya kufuta utambulisho wa Kiislamu na Ukristo katika Quds tukufu na badala yake kulipa eneo hilo utambulisho bandia wa Kizayuni.

3462394

captcha