IQNA

Kongamano la Miujiza ya Qur'ani Lafanyika Misri

11:21 - April 08, 2017
Habari ID: 3470923
TEHRAN (IQNA)- Kongamano la 23 la Ijaz (miujiza) katika Qur'ani Tukufu na Sunna ya Mtume SAW limefanyika wiki hii nchini Misri.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kongamano hilo la kitaalamu limefanyika katika Chuo Kikuu cha Al Wadi Al Junub katika mkoa wa Qena nchini Misri kwa ushirikino wa Jumuiya ya Kimataifa ya Miujiza ya Kisayansi ya Qur'ani Tukufu na Sunnah.

Wasomi, wanazuoni na wanafikra kutoka maeneo mbali mbali ya Misri waliwasilisha makala katika kongamano hilo kuhusu maudhui za miujiza ya Qur'ani Tukufu.

Halikadhalika pembizoni mwa kongamano hilo kumefanyika mashindano ya kuhifadhi Qur'ani na Hadithi za Mtume SAW.

Lengo kuu la kongamano hilo la kila mwaka limetajwa kuwa ni kuwahimiza wasomi kufnaya utafiti wa kisayansi kuhusu miujiza ya Qur'ani Tukufu na Sunnah katika nyuga mbali mbali za sayansi kama vile tiba, uhandisi, biolojia, falaki, jiolojia pamoja na sayansi za kijamii na kidini.


captcha