IQNA

Harakati za Qur'ani Tukufu

Semina ya Miujiza ya Kimatibabu ya Quran Yafunguliwa Gaza

22:21 - March 15, 2023
Habari ID: 3476710
TEHRAN (IQNA) – Toleo la tano la semina kuhusu miujiza ya kimatibabu ya Qur'ani Tukufu ilianza katika Mji wa Gaza.

Bodi ya Miujiza ya Qur'ani Tukufu na Sunnah ya Mtume Muhammad (SAW), yenye mafungamano na Kituo cha Qur'ani cha Chuo cha Osul Deen Gaza , imeandaa hafla hiyo ya kielimu kwa ushirikiano na kitivo cha sayansi ya matibabu cha Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Gaza.

Idadi kubwa ya wasomi, wanafikra, watafiti na wahubiri kutoka vyuo vikuu mbalimbali wanashiriki katika semina hiyo.
Aliyan al-Hululi, afisa wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Gaza amesema katika sherehe za ufunguzi kuwa semina hiyo inalenga kustawisha sayansi ya Kiislamu na kuangazia vipengele tofauti vya miujiza ya Qur'ani Tukufu katika uga wa tiba.
Uumbaji wa Adamu na Hawa na marufuku ya Qur'ani Tukufu  kula nyama ya nguruwe na wanyama waliokufa zilikuwa mada zilizojadiliwa katika siku ya kwanza ya semina.
Qur'ani Tukufu si kitabu cha sayansi wala lengo lake si kupanua mipaka ya sayansi. Lakini ni kitabu kinachojibu maswali ya watu kuhusu masuala ya sayansi. Kuna aya nyingi zinazozungumzia masuala ya kisayansi, zikiwemo kuhusu uumbaji wa mwanadamu.
Katika miaka ya hivi karibuni, makala nyingi kuhusu miujiza ya kimatibabu ya Qur'ani Tukufu katika nyanja kama vile embryology, ngozi na anatomy ya ubongo zimechapishwa katika nchi tofauti na Waislamu na vile vile wanazuoni wasio Waislamu.

4128301

captcha