IQNA

18:37 - October 31, 2018
News ID: 3471725
TEHRAN (IQNA)- Jeshi la Nigeria limeua shahidi Waislamu 34 waliokuwa wakishiriki katika maadhimisho ya Arobaini ya Imam Hussein AS.

Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) imesema kuwa, watu 35 wameuawa shahidi baada ya jeshi la Nigeria kushambulia mkusanyiko wa Waislamu wa madhehebu ya Shia waliokuwa katika maadhimisho ya ya Arobaini ya Imam Hussein AS katika mji mkuu wa nchi hiyo, Abuja. Hatahivyo Jeshi la Nigeria limedai kuwa ni watu watatu waliouawa.

Shambulio hilo ni mlolongo wa mashambulio ya jeshi la Nigeria dhidi ya Waislamu Mashia ambapo katika shambulio jingine kama hilo siku ya Jumamosi kwa akali waombolezaji zaidi ya 14 wa Arobaini ya Imam Hussein AS waliuuawa shahidi katika meneo mengine

Kwa msingi huo, idadi ya Waislamu wa Kishia waliouawa shahidi na jeshi la Nigeria hivi karibuni imeongezeka na kufikia mashahidi 49.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limebainisha masikitiko yake kufuatia hatua ya Jeshi la Nigeria kuwafyatulia risasi Waislamu.

Ibrahim Mussa, msemaji wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa, matembezi ya Arobaini ya Imam Hussein AS yalikwenda sambamba na maandamano ya kutaka kuachiliwa huruu Sheikh Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa harakati hiyo.

Sheikh Zakzaky na mkewe walitiwa nguvuni tarehe 13 Desemba 2015 wakati askari wa jeshi la serikali ya Nigeria waliposhambulia Husainiyah ya Baqiyatullah katika mji wa Zaria, jimboni Kaduna kaskazini mwa nchi hiyo.

Siku walipomtia nguvuni Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe, askari wa jeshi la Nigeria waliwafyatulia risasi waumini waliokuwa wamekusanyika kwenye Husainiyah hiyo na mbele ya nyumba yake, wakawaua shahidi Waislamu mamia kati yao wakiwemo watoto wake watatu wa kiume.

Wananchi Waislamu wa Nigeria wameshaandamana mara kadhaa katika miji mbalimbali ya nchi hiyo kutaka kiongozi huyo wa kidini aachiliwe huru.

Majlisi na matembezi ya siku ya Arobaini hufanyika kila mwaka tarehe 20 Safar, kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria, baada ya kupita siku Arobaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram, kwa ajili ya kukumbuka siku aliyouawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbalamwaka 61 Hijria Qamaria. Haram Takatifu ya Imam Hussein AS iko katika mji huo wa Karbala.

3467115

Tags: iqna ، waislamu ، nigeria ، arobaini
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: