Mkutano huo wa siku tatu ambao ulianza Jumatatu umewaleta pamoja washiriki 1,000 wakiwemo wanazuoni wa kidni, wasomi na wanafikra kutoka nchi mbali mbali. Mada kuu ya kongamano la mwaka huu ambali limefanika mjini Abu Dhabi ni 'Nafasi ya Dini katika Kueneza Kustahamiliana'.
Akihutubu katika ufunguzi wa kikao hicho Waziri wa Masuala ya Kustahamiliana nchini UAE Sheikh Nahyan bin Mubarak Al Nahyan alisisitiza umuhimu wa kuhurumiana watu kutoka tamaduni na dini mbali mbali. Amesema UAE inaamini kuwa kustahamiliana ni kati ya mafunzo ya dini tukufu ya Kiislamu.