IQNA

13:19 - November 14, 2019
News ID: 3472215
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko mstari wa mbele katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani katika kuwatetea watu wa Palestina.

Rais Rouhani: Iran iko mstari wa mbele kuunga mkono taifa la Palestina

Rais Hassan Rouhani ameyasema hayo Alhamisi asubuhi mjini Tehran wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 33 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu na kuongeza kuwa, Palestina na Quds Tukufu ni maudhui mbili muhimu zaidi katika Ulimwengu wa Kiislamu hivi leo. Rais Rouhani ameashiria sera za Marekani na utawala wa Kizayuni za kutaka kadhia ya Palestina isahaulike na kusema: "Ulimwengu wa Kiislamu hautawaruhusu maadui  kusahaulisha kadhia ya Palestina ambayo ni kadhia ya kwanza katika Ulimwengu wa Kiislamu."

Ameashiria kufeli kwa siasa za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na mwamko na kuwa macho ulimwengu wa Kiislamu na kusema: Mauaji ya raia madhlumu wa Afghanistan, mauaji ya watu wa Iraq na raia wanaodhulumiwa wa Yemen, na kuzusha hitilafu na mifarakano katika nchi za Waislamu ni baadhi tu ya matokeo ya njama habithi za Marekani katika eneo hili.

Rais Rouhani amesisitiza kuwa Palestina inapaswa kukombolewa na Wapalestina na Waislamu shupavu na kuongeza kuwa: Kizazi cha vijana kinapaswa kutambua kuwa, Marekani sio na haiwezi kuwa rafiki wa mataifa ya eneo hili na Waislamu; hivyo masuala ya kieneo yanapaswa kutatulia na wakazi wake.

Rais wa Iran ameeleza masikitiko yake kutokana na mwenendo wa baadhi ya nchi za Waislamu wa kufanya mapatano na utawala wa Kizayuni wa Israel na kutumia suhula za kijasusi za utawala huo dhidi ya mataifa ya Waislamu na kambi ya mapambano.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ameongeza kuwa, "Kizazi cha vijana kinapaswa kutambua kuwa, Marekani haijawahi kuwa na haitakuwa rafiki wa mataifa ya eneo na Waislamu na utatuzi wa matatizo ya eneo unapaswa kuwa mikononi mwa wananchi na Palestina inapaswa kukombolewa na Wapalestina na Waislamu mashujaa katika eneo."

Mkutano wa 33 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu umeanza leo Alkhamisi hapa mjini Tehran kwa kaulimbiu ya "Umoja wa Umma wa Kiislamu katika Kulinda Msikiti wa al Aqsa". Mkutano huo unaohudhuriwa na wasomi, wanasiasa, wahadhiri wa vyuo vikuu na wanafikra 400 kutoka nchi 90 duniani.   

Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu imeandaa Mkutano wa 33 wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu ambao umepangwa kufanyika katika mji mkuu wa Iran, Tehran, kuanzia Novemba 14-16. Kongamano hilo hufanyika kila mwaka katika Wiki ya Umoja wa Waislamu.

3856932

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: