IQNA

11:45 - December 20, 2019
News ID: 3472288
TEHRAN (IQNA) - Mkuu wa Misri, Cairo na mji wa kale wa Bukhara nchini Uzbekistan imetangazwa kuwa miji mikuu ya utamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu mwaka 2020.

Hayo yametangazwa huko Tunis, Tunisia katika kikao cha Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni (ISESCO).
Mkurugenzi Mkuu wa ISESCO Salim bin Muhammad al Malik amesema lengo la kuteua miji mikuu ya utamaduni ni kustawisha utamaduni katika nchi za Kiislamu.
Mji wa Tunis ndio uliokuwa mji mkuu wa utamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu mwaka 2019 na ulichaguliwa kutokana na historia yake ndefu ya Kiislamu.
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Utamaduni Tunisia Mohammad Zeynulabidi amesisitiza kuhusu umuhimu wa kustawisha sera za utamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu.
ISESCO ni taasisi ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kiislamu OIC na ilianzishwa Mei mwaka 1979. ISESCO ndio taasisi kubwa zaidi ya Kiislamu katika uga wa kimataifa inayoshughulikia masuala ya elimu, sayansi na utamaduni.

3865054

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: