Mohammad Hossein Ansari aliyasema hayo katika hafla iliyofanyika kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Sanaa ya Kiislamu katika Kituo cha Utamaduni cha Iran mjini Sarajevo mapema wiki hii.
Alisema kuwa kwa karne nyingi wasanii wa Kiislamu walijitahidi kueneza maadili matukufu ya Kiislamu na ya kibinadamu kupitia lugha ya sanaa.
Ameongeza kuwa Uislamu hauna ujumbe wowote zaidi ya kuwalingania watu kumwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Salma Pandjic, mtaalam wa sanaa ya Kiislamu wa Bosnia, pia alihutubia sherehe hiyo. Aliashiria Hadhithi ya Mtume (SAW) isemayo "Mungu ni mzuri na anapenda uzuri", na akasema Hadithi hii inaweka wazi msimamo wa Uislamu juu ya uzuri na sanaa.
Kulingana na mtaalamu huyo, maumbile yamekuwa chanzo kikuu cha msukumo kwa wasanii wa Kiislamu.
Siku ya Kimataifa ya Sanaa ya Kiislamu ilitangazwa katika kikao cha 40 cha Mkutano Mkuu wa UNESCO mnamo 2019 na hufanyika kila mwaka mnamo Novemba 18.
Inalenga kuongeza ufahamu wa maneno ya kisanii ya zamani na ya kisasa ya Uislamu, na mchango wa utamaduni kupitia sanaa ya Kiislamu kwa ustaarabu.
3490785