IQNA

Marekani yatoa tishio la kumuua kamanda mpya wa Kikosi cha Quds cha IRGC

13:39 - January 23, 2020
Habari ID: 3472399
TEHRAN (IQNA) - Mwakilishi maalumu wa Marekani katika masuala ya Iran ametoa matamshi ambayo yanashiria utambulisho wa kigaidi wa serikali ya Washington ambapo amezungumza kuhusu kumuua kamanda aliyechukua nafasi ya kamanda Muirani Shahidi Luteni Jenerali Qasem Soleimani.

Brian Hook mkuu wa kitengo cha hatua dhidi ya Iran katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani katika mahojiano aliyoyafanya Alhamisi na gazeti la Asharq al-Awsat pembizoni mwa mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani huko Davos, Uswisi ametoa tishio dhidi ya kamanda mpya wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Brigedia Jenerali Ismail Qaani.

Afisa huyo wa Marekani amedia kuwa iwapo, Brigedia Jenerali  Qaani  atafuata njia ya Shahidi Luteni Qassim Soleimani basi atakuwa na hatima sawa  iliyomkumba kamanda huyo wa zamani wa Kikosi cha Quds cha IRGC.

Hook katika kuendeleza vitisho vyake vya kumuua Brigedia Jenerali Qaani amedai kuwa, Trump ameamua kuwa, atatoa jibu kwali kwa hujuma yoyote dhidi ya Wamarekani.

Mkuu huyo wa kitengo cha hatua dhidi ya Iran katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ameendelea kwa kutoa matamshi ya kijuba na kudai kuwa: "Hili si tishio jipya!"

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC, Ijumaa Alfajiri 3 Januari aliwasili nchini Iraq kufuatia mwaliko rasmi wa wakuu wa nchi hiyo. Punde baada ya kuwasili, akiwa ndani ya gari pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, Naibu Kamanda wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq maarufu kama al Hashd al Shaabi pamoja na watu wengine wanane, walishambuliwa tokea angani na wanajeshi vamizi na wa kigaidi wa Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad na wote wakauawa shahidi katika tukio hilo.

Kufuatia ugaidi huo wa Marekani usiku wa kuamkia Jumatano 8 Januari, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC lilizipiga kwa makumi ya makombora, kambi mbili za Marekani nchini Iraq ikiwa ni kujibu jinai ya kigaidi iliyofanywa na askari vamizi wa Marekani ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC.

3873661

captcha