IQNA

17:31 - March 15, 2020
News ID: 3472567
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Zawadi ya Al Qasimia katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) yameakhirishwa ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama kirusi cha corona.

Wasimamizi wa mashindano hayo wanasema uamuzi huo umechukuliwa ili kulinda afya ya umma na kusaidia jitihada za kitaifa za kuzuia kuenea COVID-19.

Kila miaka miwili Chuo Kikuu cha Al Qasimia cha Sharjah huandaa mashindano hayo ya kimataifa ya Qur’ani na Sunnah kwa ajili ya wanafunzi wa kike na kiume wa vyuo vikuu vya UAE na nchi zingine duniani.

Mashindano hayo huandaliwa katika kategoria kadhaa za kuhifadhi Qur’ani Tukufu na Sunnah ya Mtume SAW. Mashindano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika kuanzia Aprili 16. Tarehe mpya ya mashindano hayo itatangazawa baadaye.

3885116

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: