IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Ni mwanadamu yupi mwenye akili atakubali msaada wa Marekani ambayo imetuhumiwa kuunda kirusi cha corona

15:36 - March 22, 2020
Habari ID: 3472592
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Marekani haiaminiwi hata kidogo na kuongeza kuwa: "Wakati Marekani inatuhumiwa kutegeneza kirusi cha corona, ni mwanadamu yupi mwenye akili atakubali msaada wa nchi hiyo."

Ayatullah Sayyed Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo Jumapili katika hotuba ya moja kwa moja kwa njia  ya televisheni ambapo ameashiria matamshi ya wakuu wa Marekani ambao wamedai mara kadhaa kuwa wako tayari kutuma misaada ya dawa na tiba iwapo Iran itawasilisha maombi. Kiongozi Muadhamu amesema: "Kauli za Wamarekani ni kati ya matamshi ya ajabu sana kwa sababu wenyewe wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa dawa na vifaa ya kitiba vya kuzuia ugonjwa huu na hata baadhi ya wakuu wa nchi hiyo wamezungumzia upungufu wa kuogofya. Kwa msingi huo, iwapo wana uwezo, kwanza wawasaidie watu wao."

Ayatullah Khamenei amesema matamshi ya wakuu wa Marekani hayakubaliki na kuongeza kuwa: "Yamkini Wamarekani wakatuma dawa ambazo zitapelekea corona kuenea zaidi au kudumu zaidi au hata pengine wakawatuma watu kwa anuani ya matabibu ili waje kuona taathira ya virusi ambavyo inasemekana baadhi vimeundwa tu kwa ajili ya muundo wa kijenetiki wa Wairani Iran." Ameongeza kuwa yamkini Marekani ikawatuma matabibu hao ili pia waje kukamilisha  taarifa zao na wazidishe uhasama wao dhidi ya Iran.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika sehemu nyingine ya hotuba yake amesisitiza kuwa, 'subira na istikama' pamoja na kutumia akili, tadibiri na mashauriano ni nukta ambazo zitapelekea kupatikana ushindi kamili.' Ameendelea kusema kuwa,  subira maana yake si kusalimu amri au kukaa bila kufanya chochote na wala subira haina maana ya kuwa dhaifu  bali maana yake ni kusimama mbele ya adui kwa ushujaa na tadbiri ili kumshinda.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria uzoefu wa miaka 40 na uwezo mkubwa wa Iran katika kukabiliana na changmoto na matatizo na kisha akalihutubu taifa la Iran kwa kusema: "Nchi hii ina uwezo mkubwa na jambo muhimu ni wakuu wa nchi kutambua uzoefu huu na kisha katika sekta zote kuwatumia vijana waumini, wenye motisha na walio tayari kufanya kazi."

Ayatullah Khamenei kwa mara nyingine ametoa wito kwa wananchi kuzingatia na kulipa uzito suala la maagizo ya  Idara ya Kitaifa ya Kukabiliana na Corona huku akielezea matumaini kuwa, "Mwenyezi Mungu SWT ataondoa balaa hii haraka katika taifa la Iran, mataifa ya Waislamu na wanadamu wote."

3886882/

captcha