IQNA

Vita dhidi ya janga la corona

Jeshi la Iran laandaa 'Gwaride la Walinzi wa Nchi na Wasaidizi wa Afya'

13:37 - April 17, 2020
Habari ID: 3472673
TEHRAN (IQNA)- Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima hulinda kiwango cha uwezo wake wa kiulinzi na kumzuia adui na wakati huo huo huwa pamoja na wananchi wakati wa maafa au majanga na huwasaidia katika kutatua matatizo yao.

Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kila mwaka tarehe 29 Farvardin kwa kalenda ya Kiirani sawa na 17 Aprili huandaa gwaride katika maeneo yote ya Iran ya Kiislamu ambapo huonyesha mafanikio yake ya kiulinzi na kijeshi kwa mnasaba wa 'Siku ya Jeshi'. Mwaka huu, kufuatia kuibuka ugonjwa wa corona au COVID-19, Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limeandaa 'Gwaride la Huduma' ambapo nara na kauli mbiu ni 'Walinzi wa Nchi na Wasaidizi wa Afya' kote katika Iran ya Kiislamu.

Katika 'Siku ya Jeshi' vifaa mbali mbali vimezinduliwa ambayvo vina umuhimu kwa mtazamo wa kijeshi na pia kwa afya ya jamii katika kukabiliana na corona. Katika gwaride mbali mbali kote Iran, Jeshi la Iran limeonyesha vifaa ya kuangamiza virusi, hospitali zinazoweza kuhamishwa, na magari ya deraya yenye vifaa vya kijeshi ambayo yanatumika katika vita dhidi ya corona.

Kufanyika gwaride na mazoezi ni jambo la kawaida katika shughuli za kila mwaka  katika majeshi yote duniani na kwa msingi huo, katika 'Siku ya Jeshi', Jeshi la Iran huonyesha sehemu ndogo tu ya uwezo wake wa kujihami na kumzuia adui sambamba na kuzindua mafanikio na zana za kisasa ambazo zimeundwa hapa nchini.

Kuhusiana na nukta hii,Brigedia Jenerali Kioumars Heydarikamanda wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Iran ameashiria msaada wa Jeshi la Iran kwa wananchi katika kipindi hiki cha kukabiliana na janga la corona na kusema: "Jeshi la Iran halichochei vita na stratijia ya pamoja na nara ya Jeshi ni kuwahudumia wananchi."

Sambamba na kuibuka ugonjwa hatari wa corona, Jeshi la Iran lilianza kutekeleza stratijia ya hujuma na kwa kutumia uwezo wake mkubwa linaendelea kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 na leo  'Gwaride la Huduma' ni misdaki ya kwazi ya kutumia uwezo wote wa Jeshi la Iran katika kulinda maisha ya wananchi mkabala wa adui anayejulikana kama corona.

3892131

captcha