IQNA

Zarif katika mhojiano na Folha de S.Paulo
19:24 - March 21, 2020
News ID: 3472587
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Mambo ya Nje wa amesema kuwa, ugaidi wa kimatibabu wa Marekani unatatiza mapambano athirifu dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo vinavyoenea kwa kasi duniani.

Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameyasema hayo katika mazungumzo na gazeti la Folha de S.Paulo linalochapishwa nchini Brazil kuhusiana na mapambano ya wananchi wa Iran dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 au virusi vya corona. Katika mahojiano hayo yaliyochapishwa leo Jumamosi, Zarif ameongeza kuwa vikwazo haramu na vya upande mmoja vya Marekani vinaizuia Iran kupata dawa na vifaa vya matibabu na kuongeza kuwa: Makampuni yanayotengeneza zana za tiba ya Ulaya hayafanyi biashara na Iran kutokana na vitisho vya Marekani.

Zarif amesema, katika mtazamo wa sheria, hatua hiyo inatambuliwa kuwa ni jinai dhidi ya binadamu na kuongeza kuwa, ugaidi wa kiuchumi wa Marekani unapaswa kusitishwa, na nchi nyingine pia hazipaswi kukubali sera za kibeberu za Marekani kwa matarajio kwamba hazipatwi na madhara yoyote.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia ameashiria jibu la wananchi wa Iraq baada ya askari magaidi wa Marekani kumuua Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Abu Mahdi al Muhandes na wenzao kadhaa na kusema: Iwapo Wamarekani wataendeleza uchokozi huo dhidi ya taifa la Iraq wanapaswa kusubiri majibu zaidi ya Wairaqi.

Vilevile amezungumzia jibu la makombora ya Iran dhidi ya kambi ya jeshi la Marekani nchini Iraq baada ya muaji ya kigaidi ya Kamanda Soleimani na kusema: Jibu la serikali ya Iran ambalo lilikuwa hatua ya kujilinda dhidi ya kambi iliyotumiwa kumshambulia Luteni Jenerali Qassem Soleimani, lilifanyika kwa mujibu wa kifungu nambari 51 cha hati ya Umoja wa Mataifa.   

3886770

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: