IQNA

Asasi za Kiislamu zagawa futari Mwezi wa Ramadhani mjini New York

15:46 - May 02, 2020
Habari ID: 3472726
TEHRAN (IQNA) – Asasi za Kiislamu mjini New York nchini Marekani zimeungana na kuanzisha mpango wa kugawa futari kwa wasiojiweza katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kinyume na Ramadhani ya miaka iliyopita, misikiti kote duniaini imefungwa sawa na maeneo ya iabda ya dini nyiginezo na waumini wametakiwa wabakia majumbani mwao ili kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.

Kutokana na hali hiyo, Waislamu wanakabiliwa na changamoto ya kupata chakula halali kote Marekani.  Kwa msingi huo asaki za Kiislamu mjini New York zimeungana na zinagawa vifurishi 1,000 vya futari kila siku katika Mwezi wa Ramadhani katika mitaa kadhaa ikiwemo Brighton Beach, Midwood, Bay Ridge na Queens.

Mohammad Bahe, muanzisihi wa asasi inayojulikana kama Muslims Giving Back anasema, “hapa tunaona faidi ya asazi mbali mbali kuungana kwa ajili ya kuhudumua jamii.

Kati ya jumuiya za Waislamu ambazo zimeungana katika kutoa futari mjini New York ni pamoja na Pakistani American Youth Society (PAYS), Muslims Giving Back (MGB), NYPD Muslim Officers Society, Khyber Society of America, Innayah Services Inc., Shorefront Coalition na Gyro King.

3471325

captcha