IQNA

Uislamu duniani

Mwezi wa Kimataifa wa Historia ya Waislamu Kuadhimisha Mafanikio ya Waislamu

22:23 - May 21, 2022
Habari ID: 3475274
TEHRAN (IQNA)- Mwezi wa Kimataifa wa Historia ya Waislamu ni mpango wa kila mwaka unaoadhimisha mafanikio ya Waislamu katika historia na kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu duniani kote kupitia elimu.

Waandalizi wanasema tukio hili la kimataifa mwaka huu limekuwa na ushiriki wa kiwango cha juu kupitia mitandao ya kijamii.

Mwezi wa Kimataifa wa Historia ya Waislamu, ambao ulianzishwa na Shirika la Siku ya Hijabu Duniani lenye makao yake mjini New York mwaka wa 2021 na ambalo umeadhimishwa Mei, unalenga kutambua na kuongeza ufahamu wa wasomi Waislamu ambao wamekuwa na mchango mkubwa wa kihistoria katika kustawisha jamii wa mwanadamu.

Shirika hilo linasema kuwa maadhimisho hayo, ambayo yanalenga shule, vyuo vikuu, mahali pa kazi, biashara, mashirika, na maeneo kijamii, ni sherehe ya kila mtu, bila kujali kabila au dini.

Zaidi ya wawakilishi wa nchi 26 walishiriki katika uzinduzi wa  Mwezi wa Kimataifa wa Historia ya Waislamu miezi 12 iliyopita lakini mwaka huu idadi hiyo imeongezeka kwa kiasi kikubwa, Shirika la Siku ya Hijabu Duniani limesema, huku watu binafsi zaidi, mashirika, wafanyabiashara na taasisi za elimu wakishiriki.

"Kwa kuongeza, tumeona kuongezeka kwa ufahamu wa Mwezi wa Kimataifa wa Historia ya Waislamu kwenye mitandao ya kijamii kwa watu binafsi na wasomi, (na) ufikiaji wetu kwenye mitandao ya kijamii umeongezeka mara nne kutoka mwaka jana," taarifa hiyo imeongeza..

Shirika hilo - ambalo lilianzisha Siku ya Hijabu Duniani, inayoadhimishwa Februari 1 kila mwaka ili kueneza ufahamu wa vazi la Hijabu na kwa nini inavaliwa - lilisema lengo lake lilikuwa ni Mwezi wa Kimataifa wa Historia ya Waislamu kutambuliwa nchini Marekani, na kimataifa, ili kusaidia kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu duniani kote.

Jiji la New York ilipitisha azimio la kutambua Mwezi wa Kimataifa wa Historia ya Waislamu  mnamo Mei 4, 2021, " ili kuwaenzi wale wanaokuza maelewano ya tamaduni mbali mbali jambo ambalo linaimarisha maelewano baina ya jamii zinazoishi  katika  Jimbo la New York," Andrew Cuomo, gavana wakati huo, alisema.

Shirika la Siku ya Hijabu Duniani  limekuwa likitoa wito kwa viongozi  duniani kote kuiga mfano huo wa Cuomo. Pia linawahimiza watu binafsi, mashirika, na taasisi za elimu kuhusika na kusaidia kuongeza ufahamu wa kampeni hiyo.

Njia ambazo Waislamu na wasio Waislamu wanaweza kushiriki ni pamoja na ushiriki wa mitandao ya kijamii, kuwasihi maafisa wa serikali kuutambua mwezi wa Mei kama Mwezi wa Kimataifa wa Historia ya Waislamu, kuunga mkono biashara za Kiislamu au kutoa michango kwa mashirika la Kiislamu, kusoma wasifu wa Mwislamu mashuhuri au kupinga wazi wazi ubaguzi na chuki dhidi ya Waislamu katika jamii.

Kaulimbiu ya tukio la mwaka huu inalenga kuwaarifisha wasomi Waislamu wa zama hizi na wale za zame za kale maarufu kama  ‘Zama za Dhahabu Kiislamu’ ambapo Waislamu walitia fora katika sekta sekta nne za elimu, STEM (sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati); sanaa huria; na uvumbuzi. Mikutano imeandaliwa kila wiki ili kuongeza ufahamu wa watu muhimu katika nyanja hizi.

"Katika mkutano wa kwanza, watoa mada walijadili mifano ya Ibn Sina (Avicenna), baba wa tiba ya kisasa, kutoka ‘Enzi ya Dhahabu’, na pia wamewaangazia Dk. Ugur Sahin na Dk. Ozlem Tureci, Waisalmu wenye asili ya Uturuki ambao ni waanzishaji wa BioNTech, kampuni inayolenga kutengeneza chanjo ya saratani kwa ushirikiano na Pfizer. BioNTech pia ilitengeneza chanjo ya COVID-19,” imesema taarifa ya na Shirika la Siku ya Hijabu Duniani

Waislamu wengine mashuhuri walioangaziwa mwaka huu ni pamoja na mshairi Muirabu wa karne ya 13, Rumi, mshairi wa Kiarabu wa karne ya sita Imru' Al-Qais, daktari mpasuaji wa mfumo wa neva Mpakistani-Mmarekani Dk. Ayub Ommaya, mwanabiolojia wa molekuli wa Palestina-Jordan Dk. Rana Dajani, mwanafalsafa Mwarabu Ibn Khaldun. , msafiri maarufu Morocco Ibn Battuta, na mwanaanga wa Kituruki Burcin Mutlu-Pakdil, miongoni mwa makumi ya wengine.

Shirika la Siku ya Hijabu Duniani pial imeshirikiana na mashirika tofauti ikiwa ni pamoja na Majlis Ash-Shoura: Baraza la Uongozi la Kiislamu la New York, shirika mwamvuli ambalo linawakilisha zaidi ya misikiti na mashirika 90 ya Kiislamu.

"Katika miongo miwili iliyopita, Waislamu kwa ujumla vyombo vya habari vimewasilisha taswira hasi ya Waislamu," mwanzilishi na afisa mkuu mtendaji wa Mwezi wa Kimataifa wa Historia ya Waislamu, Nazma Khan, alisema.

Akiwa amekulia huko New York, alisema kwamba mvuto wake umetokana na kuona " kutojumuishwa kwa historia ya Uislamu na Waislamu katika mtaala jumla wa shule."

3478992

captcha