IQNA

Ayatullah Araki awatumia ujumbe vijana wanaopigania haki na uadilifu duniani

10:59 - June 20, 2020
Habari ID: 3472879
TEHRAN (IQNA) – Ayatullah Muhsin Araki, mwanachama wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu Iran, amewatumia ujumbe wa video vijana wanaoandamana kote duniani hakitaka haki na uadilifu duniani.

Katika ujumbe huo ambao hasa umewalenga vijana wa Marekani wanaopinga ubaguzi wa rangi, Ayatullah Araki amepongeza harakati za hivi karibuni za wananchi wa Marekani na kusema watu wote duniani wanaunga mkono jitihada zao za kutaka uadilifu.

AIdha amesema mwamko wa Wamarekani ambao umeshuhudiwa katika maandamano ni mwamko wenye baraka na unaopigani uadilifu. Ameelezea matumaini yake kuwa mwamko huo utapelekea kuwepo uadilifu na uhuru duniani na kuondolewa udhalimu na ukandamizaji wa utawala wa kibepari wa Marekani na vibaraka wake. Amesema utawala huo wa kibepari wa Marekani kwa karne kadhaa sasa umwazuia watu dunaini kupumua.

3471739

Kishikizo: araki marekani Floyd
captcha