IQNA

12:19 - June 22, 2020
News ID: 3472887
TEHRAN (IQNA) – Tarehe 20 imesadifiana na mwaka wa 50 tokea alipoaga dunia Mohamed Siddiq El-Minshawi aliyekuwa na lakabu ya 'qarii wa maqarii' ambaye hadi sasa amesalia kuwa miongoni mwa wasomaji wakubwa wa Qur'ani duniani.

El-Minshawi alizaliwa Januari 1920 katika mji wa Al Minshah katika jimbo la Sohag nchini Misri na alilelewa na kuinukia katika familia ya wasomaji Qur'ani. Alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 8 na mwaka mmoja baadaya akaanza kujifunza kusoma Qur'ani kitaalamu.

Baada ya muda usio mrefu Minshawi alipata umashuhuri kama qarii ambaye alikuwa akitumia mbinu za Tarteel na Tahqiq katika usomaji wake.

Alisafiri katika nchi nyingi duniani kwa ajili ya usomaji Qur'ani zikiwemo Indonesia, Jordan, Saudi Arabia, Syria, Iraq, Pakistan na Sudan.

Misri ni mashuhuri duniani kama nchi ambayo imeweza kutoa wasomaji bora zaidi wa Qur'ani Tukufu katika miongoi ya hivi karibuni.

3905722

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: