IQNA

Qiraa ya Qur'ani Tukufu ya hivi karibuni ya Shahat Anwar + Video

15:38 - August 27, 2020
Habari ID: 3473109
TEHRAN (IQNA) – Qarii mashuhuri wa Misri, Mahmodu Shahat Anwar hivi karibuni alisoma aya za Qur'ani akiwa safarini katika jimbo la Dakahlia nchini humo.

Katika klipu hii, anasikika akisoma aya za Surah al-Mitaffifin.

Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar ni mwanae marhum Sheikh Muhammad Shahat Anwar na alizwaliwa mwaka 1984.

Alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 12 kutoka kwa baba yake. Ameweza kuibuka mshindi katika mashindano mengi ya Qur'ani ya kitaifa na kimataifa. Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar  amewahi kusafiri katika nchi nyingi duniani kushiriki katika mashindano ya Qur'ani ikiwa ni pamoja na Kuwait, Iran, Bahrain, Pakistan, Syria, Indonesia, Ufaransa, Uturuki,  Algeria na Ugiriki.

3919235

captcha