IQNA

16:51 - August 15, 2020
Habari ID: 3473070
TEHRAN (IQNA) – Klipu hii inamuonyesha qarii wa Misri Mahamoud Shahat Anwar akisoma baadhi ya aya za Surat Al-A'la za Qur'ani Tukufu bila kupumua mwaka 2016.

Imedokezwa kuwa klipu hii ilirekedoiwa nchini Kuwait na imeenezwa katika mitandao ya kijamii hivi karibuni.

Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar ni mwanae marhum Sheikh Muhammad Shahat Anwar na alizwaliwa mwaka 1984.

Alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 12 kutoka kwa baba yake. Ameweza kuibuka mshindi katika mashindano mengi ya Qur'ani ya kitaifa na kimataifa. Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar  amewahi kusafiri katika nchi nyingi duniani kushiriki katika mashindano ya Qur'ani ikiwa ni pamoja na Kuwait, Iran, Bahrain, Pakistan, Syria, Indonesia, Ufaransa, Uturuki,  Algeria na Ugiriki.

3916303

Kishikizo: qiraa ، shahat ، qurani tukufu ، misri
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: