IQNA

Sheikh Shahat Anwar akisoma aya za Surah Al-Ma'idah

18:13 - October 01, 2020
Habari ID: 3473221
TEHRAN (IQNA) – Qarii maarufu wa Misri Sheikh Mahmoud Shahat Anwar hivi karibuni alisoma aya za Qur'ani akiwa safarini katika jimbo la Dakahlia.

Akiwa katika kikao hicho cha khitma ya baba ya rafiki yake, alisoma aya kadhaa za SurAH Al Ma'idah ambayo ni surah ya tano ya Qur'ani Tukufu.

Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar ni mwanae marhum Sheikh Muhammad Shahat Anwar na alizwaliwa mwaka 1984.

Alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 12 kutoka kwa baba yake. Ameweza kuibuka mshindi katika mashindano mengi ya Qur'ani ya kitaifa na kimataifa. Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar  amewahi kusafiri katika nchi nyingi duniani kushiriki katika mashindano ya Qur'ani ikiwa ni pamoja na Kuwait, Iran, Afrika Kusini, Bahrain, Pakistan, Syria, Indonesia, Ufaransa, Uturuki,  Algeria na Ugiriki.

3926470

captcha