TEHRAN (IQNA) – Hivi karibuni kumesambazwa qiraa ya Qur'ani Tukufu ya qarii maarufu wa Misri Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar akiwa anasema aya za Qur'ani mjini Cape Town, Afrika Kusini.

Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar ni mwanae marhum Sheikh Muhammad Shahat Anwar na alizwaliwa mwaka 1984.
Alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 12 kutoka kwa baba yake. Ameweza kuibuka mshindi katika mashindano mengi ya Qur'ani ya kitaifa na kimataifa. Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar amewahi kusafiri katika nchi nyingi duniani kushiriki katika mashindano ya Qur'ani ikiwa ni pamoja na Kuwait, Iran, Bahrain, Pakistan, Syria, Indonesia, Ufaransa, Uturuki, Algeria na Ugiriki.