IQNA

Chama cha mrengo wa kulia cha Stram Kurs chaivunjia heshima Qur’ani tena Sweden

18:34 - September 11, 2020
Habari ID: 3473158
TEHRAN (IQNA) - Mjumbe wa chama chenye misimamo mikali cha Stram Kurs (Msimamo Mkali) nchini Denmark amekivujia heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani kwa kuchoma moto nakala ya kitabu hicho katika kitongoji cha wabaguzi wa rangi cha Rinkeby mjini Stockholm

Uhalifu huo umefanyika siku kadhaa baada ya chama cha mrengo wa kulia cha Stram Kurs nchini Denmark kuhujumu dini tukufu ya Uislamu katika ukurasa wake wa Facebook. 

Kiongozi wa chama hicho, Rasmus Paludan ambaye pia amewahujumu Waislamu na dini yao ametoa wito wa kufanyika mandamano dhidi ya Uislamu mjini Stockholm. 

Tarehe 28 mwezi uliopita wa Agosti pia kundi lenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia la Sweden liliitisha maandamano haramu katika mji wa Malmo na kuchoma moto nakala ya kitabu kitukufu cha Qur'ani. 

Miezi ya hivi karibuni nchi za Sweden na Denmark zimeshuhudia hujuma na mashambulizi kadhaa dhidi ya Waislamu na maeneo yao ya kidini. 

Waislamu katika nchi hizo wameeleza waswasi wao kuhusu mashambulizi hayo yanayolenga misikiti na vituo vya Kiislamu na wametoa wito wa kuzidishwa ulinzi katika maeneo hyo. 

Sambamba na hujuma hiyo dhidi ya matukufu ya Kiislamu katika nchi za Sweden na Denmark, jarida la Kifaransa la Charlie Hebdo Jumatano iliyopita, lilichapisha vibonzo vinavyomkebehi na kumvunjia heshima Mtume wa mwisho wa Mwenyezi, Muhammad SAW.

Jana Alkhamisi, wananchi wa Iran katika kona zote za nchi waliandamana kulaani kwa nguvu zao zote ufidhuli wa jarida ya Charlie Hebdo la Ufaransa wa kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW na pia kitendo cha maadui wa Uslamu cha kuchoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu katika mji wa Malmö wa kusini mwa Sweden.

Aidha Jumanne iliyopita, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alilaani vikali hatua ya jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo ya kuchapisha tena vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad (SAW) na kusisitiza kuwa: Njama hizo za Marekani na utawala wa Kizayuni ni dhambi isiyosameheka.

3472524

captcha