IQNA

Jeshi la Marekani laendelea kupora mafuta ya Syria

20:40 - September 20, 2020
Habari ID: 3473188
TEHRAN (IQNA)- jeshi la kigaidi la Marekani wameiba malori 30 ya mafuta ya nchi hiyo na kuyahamishia nchi jirani ya Iraq.

Shirika rasmi la habari la Syria SANA limeripoti kuwa, vikosi vya jeshi vamizi la Marekani, usiku wa kuamkia leo viliyaongoza malori hayo 30 ya mafuta yaliyoporwa katika eneo la Aljazira katika mikoa miwili ya Al Hasakah na Deir ez-Zur na kuyahamishia Iraq kupitia kivuko cha Al Walid.

Vikosi vya jeshi la kigaidi la Marekani, vikishirikiana na vikosi vya Wakurdi wa Syria vijulikanavyo kama Vikosi vya Kidemokrasia vya Syria SDF ndivyo vinavyodhibiti akthari ya visima vya mafuta vya Syria katika eneo la Al Jazira.

Serikali ya Syria imeshasisitiza mara kadhaa kuwa vikosi vya jeshi la kigaidi la Marekani na vikosi vyenye mfungamano navyo vilivyoko huko mashariki na kaskazini mashariki mwa nchi hiyo havina lengo jengine ghairi ya kupora mafuta ya nchi hiyo na vinapaswa kuondoka katika eneo hilo.

Jamii za makabila na kaumu mbalimbali za Syria zimekuwa zikifanya mikusanyiko na maandamano kwa muda mrefu sasa zikisisitiza kuwa muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Marekani ndio unaohusika na kuchafuka kwa amani na wizi wa mafuta unaofanywa katika mikoa ya Deir ez-Zur na Al Hasakah na zimetaka vikosi hivyo vitimuliwe katika maeneo hayo.

3472606

Kishikizo: marekani syria mafuta iraq
captcha