IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Saudi Arabia kufanyika Mwezi wa Ramadhani

13:44 - December 17, 2020
Habari ID: 3473465
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya 22 ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu nchini Saudi Arabia yatafanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika siku zitakazosadifiana na Aprili 2021.

Mashindano hayo, ambayo hujulikana kama, Zawadi ya Qur'ani ya Mfalme Salman, yalikuwa yamepangwakufanyika Machi mwaka huu lakini yaliakhirishwa kutokana na janga la COVID-19.

Wizara ya Masuala ya Kiislamu Saudia imesema mashindano hayo sasa yatafanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na yatakuwa na vitengo tafauti vya wanawake na wanaume.

Washindano watapata zawadi jumla zenye thamani ya riyali milioni 3.2

Ugonjwa COVID-19 ambao ulianza Wuhan, China Disemba mwaka jana umeaambukiza watu milioni 74 na kupelekea watu zaidi ya milioni 1.6 kupoteza maisha hadi sasa.

Ugonjwa huo umepelekea idadi kubwa ya mijumuiko ya kidini, kisiasa, na kiutamaduni kusitishwa kote duniani.

3941500

captcha