IQNA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria afariki akiwa na umri wa miaka 79

20:21 - November 16, 2020
Habari ID: 3473366
TEHRAN (IQNA) – Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Walid Muallem amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 79, shirika rasmi la habari nchini humo SANA, limeripoti.

Wizara ya mambo ya njey ya Syria imetoa taarifa na kusema Muallem amefariki Jumatatu asubuhi na ameacha wataoto watatu.

Muallem alizaliwa mwaka 1941 na kumaliza shule ya upili mwaka 1960 na miaka mitatu baadaye alihitimu akiwa na Shahada ya Awali ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Cairo.

Alianza kazi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria mwaka 1964 ambapo alihudumu kama mwanadiplomasia katika nchi kadhaa. Muallem aliteuliwa kama waziri wa mambo ya nje wa Syria mwaka 2006 na alihudumu katika nafasi hiyo hadi kifo chake. Ameandika vitabu kadhaa kuhusu uhuru, kadhia ya Palestina na Asia Magharibi.

3935452

Kishikizo: muallem syria waziri
captcha