IQNA

Mahakama ya Lahore Pakistan yaamuru Qur'ani iwe wajibu kufunzwa

10:23 - December 19, 2020
Habari ID: 3473470
TEHRAN (IQNA) –Mahakama Kuu ya Lahore, Pakistan imeamuru kuwa ni wajibu kwa taasisi zote za kielimu kuweka mafundisho ya Qur'ani katika mitaala yao kuanzia mwaka 2021.

Mahakama hiyo imetoa wito kwa wanazuoni na wasomi kubainisha maoni yao kuhusu kadhia hii ili iweze kutekelezwa katika mikoa yote nchini humo.

Mwezi Novemba, wakili mmoja aliwasilisha ombi katika mahakama hiyo kuhusu kuwa lazima ufundishwaji Qur'ani katika taasisi zote za kielimu Pakistan.

Ombi hilo lilitaka mahakama iwaamuru wahusika kuhakikisha sheria ya kushurutisha kuwepo mafundisho ya Qur'ani katika taasisi za kielimu kwa mujibu wa katiba ya Pakistan.

Wakili huyo alitaka mahakama iwaamuru wakuu wa jimbo la Punjab wajulishe shule zote za umma na za binafsi kufundisha Qur'ani kuanzia darasa la 1 hadi 12.

Mwezi Juni serikali ya jimbo la Punjab ilitangaza kuwa ni wajibu kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu kusoma tafsiri ya Qur'ani.

/3473443

captcha