IQNA

21:20 - March 19, 2021
News ID: 3473748
TEHRAN (IQNA) – Finali ya mwisho ya mashindano kitaifa ya Qur’ani Jordan imepangwa kufanyika katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa Al Mamlaka TV, mashindano hayo ya Qur’ani ambayo ni maarufu kama “Al-Hafezoun’ yameandaliwa na Wizara ya Jordan ya Wakfu, Masuala ya Kiislamu na Maeneo Matakatifu.

Wizara hiyo imetangaza kuwa duru za awali za mashindano hayo ya Qur’ani zimeshamalizika na washiriki 113 wamefanikiwa kuingia fainali.

Washiriki 29 watashindana katika finali za kuhifadhi Qur’ani kikamilifu, 34 katika kuhifadhi Juzuu 20 na 50 watashindana katika kuhifadhi Juzuu 10.

Washariki wanatazamiwa kuzingatia kanuni za kiafya za kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.

3960590

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: