Katika mashindano haya, ambayo yalihusisha washiriki 54 kutoka duniani kote. Kulingana na ripoti ya IQNA, wawakilishi wa nchi za Ufilipino, Libya, Jordan , Palestina walishika nafasi za kwanza hadi nne kwa utarajibu huo huku wawikili Ghana, na Mauritania wakishika nafasi ya tano kwa pamoja. Hussein Khani Bidgoli, mwakilishi wa Iran katika mashindano haya, alishika nafasi ya nane kati ya washiriki 54.
Kulingana na kauli ya mwakilishi wa Iran katika mashindano haya, kati ya washiriki 54, watu 18 walifanya vizuri bila makosa na kwamba ushindani kwa nafasi za juu ulikuwa mkali kati ya washiriki 10.
Jopo la waamuzi lilijumuisha wataalamu wanne wa Qur'ani kutoka nchi mwenyeji pamoja na mmoja kutoka Saudi Arabia na mmoja kutoka Misri. Mashindano yaliyofanyika kwa muda wa wiki moja kufunga yalimalizika tarehe 26 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
4274136