IQNA

Qiraa ya Qur’ani ya Sheikh Anwar Shahat mjini Kermanshah, Iran + Video

22:10 - February 09, 2021
Habari ID: 3473637
TEHRAN (IQNA) – Qiraa ya Qur’ani Tukufu ya qarii mashuhuri wa Misri Sheikh Anwar Shahat Anwar akiseoma Qur’ani Tukufu mjini Kermanshah Iran, imesembazwa katika mitandao ya kijamii.

Katika qiraa hiyo anasoma aya za Surah al Shams  katika Qur’ani Tukufu. Anwar Shahat Anwar ni mwanae marhum Sheikh Muhammad Shahat Anwar na alizwaliwa mwaka 1979.

Alifanikiwa kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu akiwa na umri wa miaka 12 kutoka kwa baba yake. Ameweza kuibuka mshindi katika mashindano mengi ya Qur'ani ya kitaifa na kimataifa. Sheikh Mahmod Shahat Muhammad Anwar  amewahi kusafiri katika nchi nyingi duniani kushiriki katika mashindano ya Qur'ani.

3953016/

 

captcha