IQNA

Kanali ya YouTube ya kufunza Qur’ani kwa lugha ya Kiswahili yazinduliwa Tanzania

21:55 - May 17, 2021
Habari ID: 3473921
TEHRAN (IQNA)- Mwambata wa Utamaduni wa Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania ametangaza kuanzishwa kanali ya YouTube ya kufunza Qur’ani Tukufu kwa wazungumzao lugha ya Kiswahili.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Bw. Morteza Pirani Mwambata wa Utamaduni  wa Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania ametangaza kuzinduliwa kanali hiyo kwa kusema: “Kanali hii ya kufunza Qur’ani Tukufu nchini Tanzania inajulikana kama “Quran in Tanzania” na imezinudliwa katika mtandao ya YouTube.” Amesema kanali hiyo ilianza shughuli zake katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo katika siku 30 za mwezi huo Mtukufu kila siku klipu za mafundisho ya Qur’ani zilikuwa zikiwekwa.

Bw. Pirani amesema kanali hiyo ya YouTube itakuwa inatoa mafunzo kwa wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili katika eneo zima la Afrika Mashariki.

Kanali hiyo mpya ya Qur’ani inapatikana katika anuani ifuatayo

www.youtube.com/channel/UC۶ZpMx_i۵XXnhQpIOapTAwg

 

3972098

captcha