IQNA

Kongamano kubwa la Qur'ani Tukufu lafanyika Dar, Tanzania

21:43 - May 26, 2025
Habari ID: 3480744
IQNA-Kongamano kubwa la Qur'ani Tukufu limefanyika jana Jumapili , Dar es Salaam Tanzania huku viongozi wa dini mbalimbali chini ya kauli mbiu 'Sauti ya Rehema'.

Mkusanyiko huo mkubwa wa Qur'ani ulianza  saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana katika Uwanja Mkubwa wa Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, ambapo kulikuwa na Tilawa ya Qur'an kutoka kwa Wasomaji Mahiri, Bingwa na Mashuhuri wa Qur'an Tukufu kutoka nchini Iran na Tanzania.

Tofauti na makongamano mengine yaliyowahi kufanyika siku kadhaa zilizopita, kongamano la jana liliweza kuwa ni la aina yake na la kipekee baada ya kukusanya watu wa dini tofauti wakiwemo Waislamu na wasio Waislamu, hii ikiwa ni ishara njema inayo onesha umoja na mshikamano katika jamii, kwani jamii inafaa kuungana na kuwa pamoja katika mambo tofauti ili kuweza kusonga mbele na kuondoa bughudha na chuki zilizo pandikizwa katika jamii hiyo kwa sababu ya dini au kitu chengine.

Katika kongamano la jana lilikuwa mkusanyiko mkubwa katika mwanga wa Qur'ani Tukufu na liliweza kukusanya watu mashuhuri na wasimamizi wa vituo mbali mbali. Mgeni rasmi katika kongamano hilo alikuwa ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis. Vilevile Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Tanzania (TIC), Sheikh Jalala Hemedi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani (JMAT) Sheikh Al-Hadi Mussa, Msimamizi mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa, Tawi la i Tanzania Dkt. Ali Taqavi pamoja na msimamizi wa kituo cha Utamaduni wa wairani nchini Tanzania Dkt Maarifi.

Hafla hii ya kipekee ilihudhuriwa na maqari Hamed Shakernejad, balozi wa Qur'ani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, pamja na maqari wengine wa Iran ambao ni Ahmed Aboulqasemi, Seyyed Jalal Masoumi, pamoja na Qari kijana Mohammad Hossein Azimi na Hafidha wa Qur'ani Bi Mahna Qanbari, wakiwa pamoja na timu ya kipindi cha televisheni cha Mahfel. 

Aidha, Maqari wawili kutoka Tanzania, Iddi Shaaban na Raja Ayoub, waliwasilisha walisoma Qur’ani katika kikao hicho. Tilawa zao na ustadi wa hali ya juu wa Qur'ani ziliwavutia waumini waliokuwa wamekusanyika kwa hamasa, huku wanawake, wanaume, vijana na watoto wakipanda jukwaani kuwatia moyo na kuomba baraka kutoka kwao. 

Katika hotuba yake Mhe. Khamis Hamza Khamis, alitoa shukrani kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mchango wake katika kuandaa hafla hii ya Qur'ani na kusema: “Niliposikia kuhusu tukio hili kupitia mabango ya matangazo, niliingiwa na hamu kubwa ya kushiriki. Leo, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia fursa ya kuhudhuria hafla hii ya Qur'ani, ambapo nimeshuhudia tilawa za kuvutia za Maqari, hususan tilawa ya kijana Mohammad Hossein Azimi pamoja na Bi Mahna Qanbari, aliye hifadhi Qur'ani.” 

Aliendelea kusema kuwa hafla hii inaakisi uhusiano mzuri wa kiutamaduni kati ya Tanzania na Iran, huku wapenzi wa Qur'ani wakijitokeza kwa wingi kuthibitisha mshikamano wa kiimani. 

Pia alisisitiza kuwa taasisi za Qur'ani nchini Tanzania zinapaswa kupata nafasi ya kushiriki katika hafla za kimataifa ili kuwawezesha Maqari na Mahafidh wake kufikia viwango vya kimataifa kama wale waliokuwa wakisoma hapa. 

Baada ya kutoa hotuba yake, Mhe. Khamis Hamza Khamis alijiunga na hafla kwa kusoma aya za Qur'ani Tukufu. 

Hafla hii ni juhudi za pamoja kati ya Taasisi ya Kimataifa ya Qur'ani na timu ya kipindi cha televisheni cha Mahfel, kwa kushirikiana na Kituo cha Kimataifa cha Qur'ani na Uenezaji wa Dini cha Shirika la Iran la Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu, pamoja na taasisi zinazoshirikiana kutoka Tanzania, ikiwemo mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha  Al-Mustafa nchini Tanzania. 

برگزاری محفل بزرگ قرآنی در دارالسلام تانزانیا + فیلم و عکس
 
برگزاری محفل بزرگ قرآنی در دارالسلام تانزانیا + فیلم و عکس
 
برگزاری محفل بزرگ قرآنی در دارالسلام تانزانیا + فیلم و عکس
 
برگزاری محفل بزرگ قرآنی در دارالسلام تانزانیا + فیلم و عکس

4284639

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu tanzania
captcha