IQNA

Utamaduni

Kitabu cha "Kabila la Washirazi Tanzania" kimechapishwa

18:05 - November 20, 2024
Habari ID: 3479784
IQNA-Ofisi ya Mwambata wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania imtayarisha na kuchapisha kitabu cha "Kabila la Washirazi Tanzania".

Kwa mujibu wa Shirika la Iran la  Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu ya Iran (ICRO), Kitabu hiki kimetayarishwa kwa lugha ya Kiingereza katika sehemu nne: "Historia ya Iran na  Uhusiano wa Iran na Afrika Mashariki", "Kuhamia Washirazi Afrika Mashariki", "Turathi ya Washiriazi Tanzania" na hatimaye "Matokeo ya Utafiti"

Kazi hii fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya hadhira ya jumla, ilizinduliwa wakati huo huo wa ufunguzi rasmi wa "Maonyesho ya Urithi wa Washirazi Tanzania" katika kipindi cha "Siku ya Utamaduni wa Shiraz".

Balozi wa Iran nchini Tanzania Hosein Alvandi alishiriki katika Siku ya Utamaduni wa Washirazi iliyofanyika jijini Dar es Salaam ili kuzidi kutia nguvu uhusiano wa kiudugu ulipo baina ya Iran na Tanzania.

Balozi wa Iran nchini Tanzania, alisema katika sherehe hizo zilizofanyika jana Jumatatu jijini Dar es Salaam kwamba, uhusiano wa nchi hizi mbili unazidi kuimarishwa na uwepo uliojaa fakhari wa Washirazi nchini Tanzania. Amehimiza kufanyika jitihada zaidi za kuhakikisha uhusiano huo unakuwa imara zaidi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Iran nchini Tanzania, Mohsen Moarefi amezungumzia miamala na mahusiano mazuri sana yaliyojitokeza baada ya Washirazi wa Iran kuelekea mashariki mwa Afrika na kusisitiza kuwa, mlahaka wa Wairan unatofautiana kikamilifu na wa wakoloni wa Magharibi ambao walizivamia nchi za Afrika ili kupora utajiri wao na hadi sasa wanajali tu maslaini yao binafsi.

Ameongeza kuwa, kutokana na Washirazi kuoanisha ada na desturi zao na mila na desturi za wenyeji wa Afrika Mashariki, wameweza kuja na utamaduni mpya wa kipekee ambao hadi leo hii wakazi wa mashariki mwa Afrika wanajivunia nao.

Wazungumzaji wengine waliohudhuria sherehe hizo nao pia wamegusia uhusiano wa kihistoria baina ya wananchi wa Iran na Waswahili wa mashariki mwa Afrika na kutilia mkazo wajibu wa kutunzwa na kuendelezwa suala hilo.

 4249000

Habari zinazohusiana
Kishikizo: washirazi tanzania
captcha