Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR), shirika kubwa zaidi la kutetea haki za Waislamu katika taifa hilo, limetoa wito huo Jumatano.
Katika podikasti hiyo, inayojulikana kama "Wavulana Wawili Wazuri wa Kiyahudi," Naor Meningher na Eytan Weinstein wanasema:
"Hakuna anayejali kuhusu mauaji ya kimbari huko Gaza. Hakuna yeyote anayejali Israel…Je, unajali ikiwa mtoto huyu wa Gaza anapata polio?.
"Pia, maadamu wako katika hali ya Nakba (maafa) kwenye mahema yao…huwezi kujizuia kufikiria kuwa inafurahisha kujua kwamba unacheza dansi katika tamasha huku mamia ya maelfu ya Wagaza hawana makazi…inafurahisha zaidi… ni tamasha la kufurahisha zaidi…
"Hivi ndivyo Waisraeli wanavyohisi….Watu wanafurahia kujua kwamba wao (Wapalestina) wanateseka."
Nakba, maana yake ni "janga au maafa" kwa Kiarabu na inahusu mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina mwaka 1948.
Pia kwenye podikasti wanasema: “Kama ungenipa kitufe cha kufuta tu Gaza, kila kiumbe anayeishi Gaza hangekuwa akiishi tena kesho. Ningebonyeza kwa sekunde moja.”
Katika taarifa, Naibu Mkurugenzi wa Kitaifa wa CAIR Edward Ahmed Mitchell alisema:
" Mashirika ya Apple na YouTube bila shaka yanngefuta podikasti hii ikiwa ingetetea waziwazi wazo la mauaji ya kimbari la kuangamiza kaumu nyingine yoyote. Haipaswi kukataka maoni ya mauaji ya kimbari dhidi ya wengine wote isipokuwa kwa Wapalestina." Amesema sheria za makampuni ya mitandao ya kijamii hazipaswi kuwa za kibaguzi huki akiongoze kuwa mashirika hayo mara kwa mara hufuta hotuba halali za kuunga mkono haki za binadamu za Palestina.”
3489774