IQNA

Waislamu wenye asili ya Afrika Marekani wampinga Harris kutokana na msimamo wa Vita vya Gaza

16:50 - October 22, 2024
Habari ID: 3479633
IQNA-Muungano wa viongozi wa Waislamu wenye asili ya Afrika nchini Marekani wamewataka wapiga kura kumkataa Makamu wa Rais Kamala Harris katika azma yake ya kuwania urais wa Marekani 2024 kutokana na sera yake ya kuunga mkono mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala dhalimu wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza.

Kundi hilo linalojumuisha takriban viongozi 50, limetoa wito wa kuungwa mkono wagombea wanaounga mkono usitishaji vita huko Gaza na kuwekewa vikwazo vya silaha dhidi ya utawala wa Israel.

Taarifa hiyo, iliyoripotiwa kwa mara ya kwanza na tovuti ya Middle East Eye, inakuja wakati utawala wa Biden-Harris ukikosolewa kwa kuunga mkono bila masharti utawala katili wa Israel wakati huu wa vita vya Gaza. Taarifa hiyo imesema: “Waislamu wanapolazimika kutetea haki na kama Waamerika wenye asili ya Afrika ambao mababu zao waliteswa na kukumbwa uhalifu mbaya zaidi, mauaji ya kimbari lazima yawe mstari wetu mwekundu. Hatuwezi kuunga mkono mgombeaji ambaye alishiriki katika mauaji ya kimbari na sasa anakataa kuweka mpango wowote wa kukomesha mauaji hayo."

Hii inaashiria mgawanyiko unaokua kati ya wapiga kura wa Kiislamu na Marekani, ambao kijadi wamekuwa wakiunga mkono wa Chama cha Democrat.

Kauli hiyo inafuatia wito wa hivi majuzi kutoka kwa mashirika ya Kiislamu yakiwataka wapiga kura kuwaunga mkono wagombea wanaotanguliza mbele kusitisha msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Israel. Hasa, kundi la Maimamu kutoka kote Marekani hivi majuzi lilitia saini barua ya kutetea kura ya mtu wa tatu, haswa katika kupinga msimamo wa Chama cha Kidemokrasia juu ya vita vya Gaza.

Kauli ya viongozi wa Waislamu Weusi pia inaangazia mshikamano wao wa kihistoria na mapambano ya Wapalestina, ikilinganisha na mapambano ya Jumuiya ya Weusi kwa haki za kiraia. "Jumuiya za watu weusi zimepigana bila kuchoka dhidi ya utumwa, ubaguzi, dhidi ya unyanyasaji wa rangi, hivyo inatambua mapambano ya Wapalestina kama vile vile kupigania uhuru, utu na haki ya kujitawala," alisema Ismahan Abdullahi, kiongozi wa Waislamu huko San. Diego na mmoja wa watia saini wa taarifa hiyo.

Kuidhinishwa kwa wagombeaji wa vyama vya tatu, haswa Jill Stein wa Chama cha Kijani, kunaonyesha vuguvugu linalokua ndani ya jamii za Kiislamu la kutoungwa mkono na Wanademokrasia.

Kulingana na upigaji kura wa hivi majuzi wa Taasisi ya Yaqeen, ni 32% tu ya Waislamu Weusi wanaonuia kumpigia kura Harris, huku asilimia kubwa ikizingatia wagombea mbadala.

"Kuna simulizi ya uwongo kwamba wengi wa Waislamu wenye asili ya Afrika wanamuunga mkono Kamala Harris," Imam Dawud Walid, kiongozi wa Waislamu wa Michigan alisema. "Inakuza mgawanyiko wa rangi kati ya Waislamu wa Amerika wakati wa mauaji ya kimbari ya kaka na dada zetu huko Gaza."

Mabadiliko haya msimamo wa wapiga kura yanakuja katika hali ambayo wapiga kura Waislamu na Wamarekani, haswa katika majimbo muhimu kama Michigan, wanaweza kuwa na jukumu muhimu katika uchaguzi ujao.

Kura za maoni zinaonyesha kuwa Harris na Rais wa zamani Donald Trump wanakaribiana, na kampeni zote mbili zinawavutia wapiga kura Waislamu na Waarabu-Waamerika.

Washington imeeleza uungaji mkono mkubwa kwa vita vya mauaji ya halaiki ya utawala wa Israel katika Ukanda wa Gaza vilivyoanza Oktoba mwaka jana.

Mashambulizi hayo ya Israel yamepelekea Wapalestina wasiopungua 42,718 kuuawa huko Gaza, wengi wao wakiwa wanawake na watoto huku takriban watu milioni 2.3 wakilazimika kuyahama makaazi yao.

3490387

captcha