IQNA

Maandamano ya kutaka Sheikh Zakzaky aachiliwe huru yaendelea Nigeria

17:32 - June 23, 2021
Habari ID: 3474033
TEHRAN (IQNA)- Wafuasi wa Sheikh Ibrahim Zakzaky kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) wamefanya maandamano nchini humo wakitaka kuachiwa huru bila ya masharti yoyote mwanazuoni huyo mtajika.

Ofisi ya Sheikh Zakzaky imetangaza kuwa, wafuasi wa mwanazuoni huyo jana walifanya maandamano katika eneo la Garki katika mji wa Abuja.

Wafuasi wa Allamah Zakzaky wamekuwa wakifanya maandamano ya amani kwa nyakati tofauti tangu baada ya maafa ya Zaria mwaka 2015. Wafuasi hao wa Sheikh Zakzaky wametaka kuachiwa huru kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria na mkewe bila ya masharti yoyote.   

Mwaka 2015 jeshi la Nigeria liliwavamia shughuli za kidini katika Husseiniya ya Imamu wa zama, katika mji wa Zaria na kuua karibu wafuasi elfu mbili wa Sheikh Zakaky waliokuwa wamekusanyika katika eneo hilo la ibada. Baada ya kumjeruhi Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe, wanajeshi wa Nigeria walimpeleka kusikojulikana. 

Sheikh Zakzaky alijeruhiwa vibaya katika hujuma hiyo ya mashambulizi ya wanajeshi wa Nigeria huko Zaria na hadi sasa jicho lake moja halioni huku lingine likikaribia kupoteza uwezo wa kuona. 

3979186

 

Kishikizo: nigeria ، sheikh zakzaky ، waislamu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :