IQNA

Jinai za Israel

Utawala wa Israel wawazuia maelfu ya Waislamu kusali Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Al-Aqsa

22:16 - January 05, 2024
Habari ID: 3478154
IQNA - Idara ya Wakfu ya Kiislamu, inayosimamia Msikiti wa Al-Aqsa huko al-Quds (Jerusalem), imesema leo kwamba ni waumini 15,000 pekee walioruhusiwa kuingia katika eneo hilo takatifu kwa ajili ya Sala ya Ijumaa kutokana na vikwazo vilivyowekwa na utawala ghasibu wa Israel.

Msikiti huo, ambao ni wa tatu kwa utakatifu katika Uislamu, unaweza kuchukua hadi waumini 300,000.

Kwa mujibu wa Idara ya Wakfu ya Kiislamu ya Msikiti wa Al Aqsa ambayo inaongozwa na Jordan, utawala huo katili uliwazuia maelfu ya Waislamu kufika msikiti huo kwa kuweka hatua kali za kiusalama karibu na Mji Mkongwe wa al-Quds na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, shirika la habari la WAFA limeripoti.

Vizuizi hivyo vimewekwa tangu Oktoba 7, wakati utawala huo ulipoanzisha vita vya mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa.

Vyanzo vya ndani viliripoti kwamba vikosi vya Israeli vilitumia mabomu ya kushtukiza, gesi ya kutoa machozi, na maji machafu kuwatawanya na kuwashambulia waumini, watembea kwa miguu na waandishi wa habari karibu na eneo la Wadi al-Joz, karibu na Jiji la Kale la Al Quds.

Watu kadhaa walijeruhiwa katika mapigano hayo. Kipande cha video kinachosambaa mtandaoni kilionyesha mwanamke akishambuliwa na wanajeshi katili wa Israel alipokuwa akijaribu kuingia msikitini kupitia lango la Al-Asbat, mojawapo ya lango kuu la kuingilia katika eneo hilo takatifu.

3486689

Habari zinazohusiana
captcha