IQNA

Nasrallah alaani hatua ya Marekani kuteka tovuti ziungazo mkono mapambano ya Kiislamu

17:29 - July 06, 2021
Habari ID: 3474074
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amelaani vikali hatua ya Marekani kuteka tovuti za vyombo vya habari vinavyounga mkono harakati za muqwama au mapambano ya Kiislamu na Iran katika eneo.

Sayyid Hassan Nasrullah ambaye alikuwa akizungumza jana katika ufunguzi wa mkutano wa "Palestina Itashinda", amesema tovuti hizo zilizotekwa na Marekani zilikuwa zinaunga mkono haki za Wapalestina na thamani za kibinaadamu.

Hivi karibuni serikali mpya ya Marekani iliendeleza sera za kiijuba ya kibeberu za nchi hiyo kwa kuzifunga tovuti za televisheni za kimataifa za Iran na vyombo vya habari vya mrengo wa muqawama au mapambano ya Kiislamu Yemen, Palestina, Iraq na Bahrain.

Televisheni ya Kiingereza ya Iran ya Press TV na zile za Kiarabu za Al Alam na Al Khauthar ni kati ya vyombo vya habari ambavyo vimefunguiwa tovuti zao na Marekani kwani zilikuwa zinaishia na kikoa cha .com ambaho humilikiwa na shirika moja la Kimarekani. Tovuti ya Press TV imesharejea katika intaneti na sasa inapatikana kupitia presstv.ir

Kiongozi wa Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrallah amesema kuna haja ya kuchukuliwa hatua za kukabiliana na njama hizo za Marekani.

Kwingineko katika hotuba yake, Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa moja kati ya malengo ya kuanzishwa kundi la kigaidi la Daesh ni kuwasahaulisha Waislamu kadhia ya ukombozi wa Palestina.

Amesema kuwa, mashambulizi yoyote yanayofanywa na Israel huwa ni mashambulizi ya Marekani, na kwamba udhibiti na ubeberu wa Marekani ni tishio kubwa zaidi kwa watu wa eneo la Magharibi mwa Asia hususan Iraq na Syria; hivyo watu wa eneo hilo wana haki ya kujiainishia mambo yao wenyewe.

Sayyid NasrAllah amesema kuwa, vyombo vya habari ni moja kati ya nyenzo muhimu za kukabiliana na adui na kwamba kusimama kidete kambi ya muqawama na mapambano ni miongoni mwa mambo yaliyochangia katika ushindi wa karibuni wa Wapalestina katika Operesheni ya Panga la Quds.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema kambi ya muqawama imeahidi kuikomboa Quds na hapana shaka kwamba itatekeleza ahadi yake.  

3475150

captcha