IQNA

Hamas: Mapambano dhidi ya Wazayuni kuendelea

14:08 - August 26, 2021
Habari ID: 3474228
TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesisitiza udharura wa kuendeleza mapambano dhidi ya utawala ghasibu wa Israel kwa kutumia suhula na nyenzo zote.

Msemaji wa Hamas Abdullatif al Qanou amesema, maandamano  yaliyofanyika jana Jumatano mashariki mwa Khan Yunis kusini mwa Ukanda wa Ghaza ni mwendelezo wa vita vya Saiful Quds vya kulilinda taifa la Palestina na matukufu yake. 

Msemaji wa harakati hiyo ya Palestina ameeleza kuwa, ni haki ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza kuishi kwa heshima na izza katika ardhi zao. Amesema, wataendeleza mapambano ili kuushinikiza utawala ghasibu wa Israel hadi pale Wapalestina watakaporejeshewa haki zao na kuvunjwa kikamilifu mzingiro dhidi ya  Ghaza. 

Jumamosi iliyopita pia makundi mbalimbali ya Palestina yalifanya maandamano karibu na ukuta wa mpakani wa mashariki mwa mji wa Ghaza kwa mnasaba wa kukumbuka kutimia mwaka wa 52 tangu kuchomwa moto Msikiti wa al Aqsa. 

Wanajeshi wa Kizayuni walitumia mabavu kukabiliana na maandamano hayo na kumuuwa shahidi Mpalestina mmoja na kuwajeruhi wengine 40 wakiwemo watoto 22. 

3475572

captcha