IQNA

INM: Sheikh Zakzaky anashikiliwa kifungo cha nyumbani

23:37 - August 28, 2021
Habari ID: 3474234
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria (IMN) Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe, Malama Zeenah Ibrahim, wanaonekana kuwa chini ya aina fulani ya kizuizi cha nyumbani.

Kiongozi huyo wa Kiislamu anataka kusafiri nje ya nchi kupata matibabu, lakini hajaweza kwenda kwani pasipoti yake na ya mkewe ingali mikononi mwa maafisa wa usalama.

Haya yanajiri wakati  wiki nne baada ya kuondolewa hatiani na kuachiliwa huru na Mahakama Kuu ya Jimbo la Kaduna.

Taarifa ya Harakati ya Kiislamu ya Nigeria (IMN) imesema maafisa wa idara za usalama Nigeria wamekanusha kumiliki hati za kusafiria za kimataifa za Sheikh Zakzaky na mke wake..

Kuna tetesi kuwa baadhi ya watendaji wenye nguvu katika katika Ofisi ya Rais Muhammadu Buhari kwa makusudi wanamnyima kiongozi wa Kiislamu haki zake.

Msemaji wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria Ibrahim Musa  ni ukweli unaojulikana hata hivyo, kwamba wakati Sheikh Zakzaky na mke wake walipokwenda India kupata matibabu mwaka 2019, kufuatia idhini ya Mahakama Kuu ya Kaduna, hati zao za kusafiri za kimataifa zilichukuliwa na maafisa wa usalam mara waliporejea nyumbani.

Aidha amekumbusha kuwa hivi sasa  hali jumla ya kiafya ya Sheikh Zakzaky na mke wake si nzuri  na kwa hivyo wanahitaji kusafiri nje ya nchi kwa matibabu.

Ameitaka serikali  kutoa hati zao za kusafiria au kuwapa mpya, mbayo itawawezesha kusafiri hadi hospitali wanayochagua bila kucheleweshwa zaidi.

Sheikh Ibrahim Zakzaky na mke wake, Mallimah Zeenah walitiwa nguvuni tarehe 13 Disemba mwaka 2015 katika shambulizi lililofanywa na jeshi la Nigeria dhidi ya kituo cha kidini cha Baqiyyatullah katika mji wa Zaria na walikuwa mahabusu kwa kipindi chote cha miaka 6 iliyopita kabla ya kuachiliwa huru mwezi Julai mwaka huu.

3475578

captcha