IQNA

Magaidi wa ISIS waua polisi 13 nchini Iraq

18:58 - September 05, 2021
Habari ID: 3474260
TEHRAN (IQNA)- Maafisa 13 wa polisi Iraq wameuawa katika shambulio la kundi la kigaidi la Daesh au ISIS dhidi ya kituo cha upekuzi barabarani kaskazini mwa nchi hiyo mapema Jumapili, vyanzo vya usalama na matibabu vilisema.

Shambulio hilo, katika eneo la Al-Rashad karibu kilomita 65 (maili 40) kusini mwa mji wa Kirkuk, lilitokea baada tu ya saa sita usiku, afisa mwandamizi wa polisi wa Iraq amewaambia waandishi habari.

"Wanachama wa Daesh walilenga kizuizi cha polisi," alisema afisa huyo, ambaye hakutaka kutajwa jina.

"Kumi na tatu waliuawa na watatu walijeruhiwa" kati ya vikosi vya usalama, afisa huyo aliongeza.

Chanzo cha matibabu kilichoko Kirkuk kilithibitisha kujiri hujuma huo. Hakukuwa na madai ya mara moja ya uwajibikaji.

Daesh iliwahi kuteka maeneo makubwa ya Iraq mnamo 2014, kabla kutimuliwa katika kampeni ya kupambana na uasi.

Serikali ya Iraq ilitangaza rasmi kushindwa kundi hilo la kigaidi  mwishoni mwa 2017, lakini mabaki ya  kundi hilo hutekeleza mashamb ulizi ya kuvizia amra kwa mara kote Iraq.

Magaidi hulenga mara kwa mara jeshi la polisi na polisi kaskazini mwa Iraq, lakini shambulio hili lilikuwa moja wapo ya hatari zaidi mwaka huu.

Mwezi Julai pia hujuma ya bomu iliyodaiwa na Daesh iliwaua watu 30 katika soko la Al-Woheilat katika kitongoji cha  Sadr, mjini Baghdad.

3475633

Kishikizo: iraq isis au daesh
captcha