IQNA

Wairani 60,000 kushiriki matembezi ya Arubaini mwaka huu

22:56 - September 13, 2021
Habari ID: 3474292
TEHRAN (IQNA)- Iraq imeafiki kuwaruhusu Wairini 60,000 kushiriki katika ziyara na mjumuiko wa siku ya Arubaini ya Imam Hussein AS mwaka huu.

Ali Reza Rashidian, mkuu wa Shirika la Hija na Ziyara Iran amesema serikali ya Iraq awali ilikuwa imeidhinisha Wairani 30,000 kushiriki matembezi ya Arubaini lakini idadi hiyo imeongezwa hadi sitini elfu wakati wa safari ya waziri mkuu wa Iraq Mustafa al Kadhimi mjini Tehran hiyo jana.

Amesema usajili wa washiriki umeshaanza na watakaoruhusiwa ni wale ambao tayari wamepokea dozi mbili za chanjo ya corona.

Iraq imesema wafanyaziara kutoka maeneo mengine duniani ni sharti waingie nchin humo kupitia viwanja vya ndege na wawe na cheti cha kipimo cha kuonyesha hawana corona.

Maadhimisho siku ya Arobaini (Arubaini au Arbaeen) hufanyika kila mwaka tarehe 20 Safar, kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Qamaria, baada ya kupita siku Arobaini tangu tarehe 10 mwezi wa Muharram, kwa ajili ya kukumbuka siku aliyouawa shahidi mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS na masahaba zake ambao walijitolea roho zao kwa ajili ya kuhuisha dini ya Mwenyezi Mungu katika jangwa la Karbalamwaka 61 Hijria Qamaria. Haram Takatifu ya Imam Hussein AS iko katika mji huo wa Karbala.

Watu wa Iraq hutembea kwa miguu kutoka miji yao ya mbali na karibu ili kufika Karbala katika siku hiyo ya Arobaini. Halikadhalika wafanyaziara kutoka nchi mbali mbali hushiriki kwa mamilioni katika hafla hiyo. Mwaka huu kutokana na vizingiti vya corona idadi ya washiriki wa Arobaini inatazamiwa kupungua.

 Siku ya Arobaini ambayo mwaka huu intazamiwa kusadifiana na Septemba 27.

3475698

Kishikizo: iran ، arubaini ، imam hussein as
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha