IQNA

Uwanja wa Ndege wa Najaf kupokea zaidi ya ndege 200 kwa siku Arbaeen inapokaribia

17:30 - August 16, 2022
Habari ID: 3475632
TEHRAN (IQNA) – Afisa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Najaf nchini Iraq amesema uwanja huo umeandaliwa kupokea zaidi ya safari 200 za ndege kila siku kuanzia siku ya kwanza ya mwezi wa Hijri wa Safar unaotazamiwa kuanza Agosti 29.

Muthanna al-Taleqani, mkuu wa ofisi ya mahusiano ya umma ya uwanja wa ndege, alisema kuwa kwa kupunguzwa kwa vikwazo vya corona, idadi kubwa zaidi ya wafanyaziara ya kidini wanatarajiwa kuwasili Najaf kwa Arbaeen mwaka huu.

Alisema uwanja huo wa ndege utakuwa na shughuli nyingi kuanzia mwanzo wa Safar kuwakaribisha wafanyaziara ya Arbaeen.

Kati ya  ndege 200 hadi 220 zinatazamiwa kutua  kila siku katika uwanja wa ndege wakati wa msimu wa Arbaeen, afisa huyo alisema.

Iran imetabiri zaidi ya Wairani  milioni 4 watekelea Iraq kwa ajili ya ziara ya Arbaeen mwaka huu, alibainisha, akiongeza kuwa kutakuwa pia na wafanyaziara wanaosafiri kwenda Najaf kutoka nchi nyingine kama Lebanon, mataifa ya Kiarabu ya Ghuba ya Uajemi na nchi za Asia.

Maadhimisho ya Arbaeen (Arubaini) ni mojawapo ya mikusanyiko mikubwa ya kidini duniani.

Siku hii huadhimishwa  siku ya 40 baada ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Hussein (AS) tarehe 10 Muharram katika Siku ya Ashura.

Kila mwaka, wafanyaziara, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri njia ndefu kwa miguu hadi Karbala, ambako ndiko kunako haram takatifu la Imam Hussein (AS).

Siku ya Arbaeen mwaka huu inasadifiana na Septemba 17 mwaka huu.

3480114

 

Kishikizo: najaf ، iraq ، arabaeen ، imam hussein as
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha