Taarifa ya idara ya mkoa wa Nangarhar imesema: “Kupitia upatanishi wa viongozi wa kikabila katika wilaya za Kot na Batkot mkoani Nangarhar, magaidi 65 wa Daesh wamejisalimisha kwa Imarati ya Kiislamu (Taliban) na wamejuta kuhusu vitendo vyao.”
Watu hao sasa wanafuatiliwa kwa karibu na wakikiuka mapatano ya kuwaachilia huru watachukuliw hatua kali, amesema Dkt Bashir, mkuu wa idara ya usalama Nangarhar.
Mkoa huo umekuwa ukishuhudia ongezeko la mashambulizi yanayotekelezwa na magaidi wa ISIS. Mapema mwezi huu serikali ya Taliban ilidai kusambaratisha ngome ya maficho ya magaidi wa ISIS mjini Kabul. Magaidi wa ISIS wamedai kuhusuika na hujuma dhidi ya misikiti ya Mashia wakati wa Sala ya Ijumaa katika miji ya Kandahar na Kunduz ambapo watu zaidi ya 100 wameuawa shahidi.