Akihutubu katika warsha iliyojadili aya za Qur'ani ambazo hutumiwa vibaya na watu wenye misimao mikali ya kidini kutetea hujuma zao dhidi yaw engine, Profesa Abdul Fattah al Awari amesema ni wajibu wa Waislamu kulinda misikiti na maeneo mengine ya ibada.
Amesema kwa mujibu wa mafundishi ya Kiislamu, ni wajibu kulina maeneo ya ibada hata yale ambayo si ya Waislamu.
Al Awari wakati mmoja walikuwa naibu mkuu wa Kitivo cha Usuluddin katika Chuo Kikuu cha Al Azhar amelaani vikali namna wale wenye misimamo mikali ya kidini wanavyofasiri vibaya aya za Qur'ani.