Jumla ya maqari au wasomaji Qur'ani Tukufu 100 kutoka nchi mbalimbali watashiriki katika duru ya shindano hilo, ambalo kauli mbiu yake ni “Zayyin al-Quran bi-Aswatikum (ipambeni Qur'ani kwa sauti zenu).
Mashindano hayo huandaliwa kila mwaka na Kijiji cha Utamaduni cha Katara kwa msaada wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar.
Jopo la majaji lilichagua walioingia fainali kutoka nchi 11 za Kiarabu na 11 zisizo za Kiarabu, zikiwemo Morocco, Algeria, Iraq, Syria, Jordan, Palestina, Lebanon, Libya na Mauritania.
Idadi ya walioingia fainali kutoka nchi zisizo za Kiarabu ni 30 mwaka huu, ikionyesha ongezeko ikilinganishwa na toleo la awali.
Khalid bin Ibrahim Al-Sulaiti, Meneja Mkuu wa Wakfu wa Kijiji cha Utamaduni, anasema Qur'ani Tukufu ni kitabu cha watu wote bila kujali utaifa na lugha zao.