IQNA

Sheikh al-Qaradaghi alaani hujuma dhidi ya Waislamu India

17:21 - October 31, 2021
Habari ID: 3474495
TEHRAN (IQNA)- Mwanazuoni wa ngazi za juu wa Kiislamu amelaani vikali hujuma za hivi karibuni dhidi ya Waislamu nchini India huku akitoa wito wa kuanzishwa harakati yakimataifa ya kutetea Waislamu ambao wanaishi kama jamii za waliowachache.

Sheikh Dkt. Ali Mohyiddeen Al-Qaradaghi katibu mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wanazuoni wa Kiislamu ametuma ujumbe wa Twitter Jumamosi kuhusu jinai wanagambo wa Kihindu wenye misimamo mikali ya kuteketeza misikiti 12 nchini India katika kipindi cha wiki moja kufuatia ongezeko la hujum dhidi ya Waislamu na kuhoji, "Ni kwa nini polisi imekaa kimya,?"

"Natoa wito wa kuundwa harakati ya kimataifa ya kisheria kwa ajili ya kulinda haki za Waislamu wanaoishi kama jamii za waliowachache maeneo mbali mbali duniani.

Ujumbe huo umekuja huku Waislamu wakiwa wanakabiliwa na wimbi jipya la hujuma nchini India. Katika baadhi ya maeneo, Wahindi wenye misimamo mikali wanawazui Waislamu kusali Sala ya Ijumaa.

Vyombo vya habari vya India vimeripoti kuwa, makumi ya Wahindu wenye misimami mikali wamekamatwa baada ya kuwazuia Waislamu kuswali Sala ya Ijumaa katika eneola Gurugum.

Ghasia za sasa dhidi ya Waislamu India zilianza pale  Wahindu wenya misimamo mikali katika jimbo la Tripura kaskazini mashariki mwa India walipowahujumu Waislamu na kuharibu misikiti kadhaa kwa sababu ya kulipiza kisasi kutokana na kile wanachodai ni kusumbuliwa Wahindu katika nchi jirani ya Bangladesh.

Jimbo la Tripura lina mpaka wa kilimota 850 na nchi ya Bangladesh ambayo wakazi wake wengi ni Waislamu. Hivi karibuni nchini Bangladesh watu waliokuwa na hasira walivamia hekalu la Wahindu ambapo watu saba walipoteza maisha katika ghasia hizo.

Machafuko hayo yaliibuka baada ya kuenea klipu iliyooneysha Msahafu ukiwe umewekwa katika goti la kijimungu cha Kihindu jambo ambalo liliwakasirisha Waislamu na kuibua ghasia katika wilaya 12 nchini Bangladesh.

Waislamu nchini India wanakabiliwa na hujuma za mara kwa mara kutoka kwa Wahindi wenye misimamo mikali tokea mwaka 2014 tokea chama cha BJP kiingie madarakani.

4009223

captcha