IQNA

Serikali ya India yatakiwa izuie hujuma za Wahindu wenye misimamo mikali dhidi ya Waislamu

22:01 - October 29, 2021
Habari ID: 3474487
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu katika jimbo la Tripura kaskazini mashariki mwa India wameitaka serikali ya nchi hiyo ichukue hatua za kuzuia magenge ya Wahindu wenye misimamko mikali kuwashambulia Waislamu na misikiti.

Kwa mujibu wa taarifa, jumuiya hiyo imesema katika siku za hivi karibuni kumeshuhudiwa hujuma ya Wahindi wenye misimamo mikali dhidi ya misikiti na makazi ya Waislamu jimboni Tripura na hivyo sasa ni dharura kuwapa Waislamu ulinzi. 

Gazeti maarufu la Hindustan Times limeandika kuwa Waislamu wamefika katika ofisi ya waziri mkuu wa jimbo la Tripura kuwasilisha malalamiko yao huku wakitaka sheria zichukuliwe dhidi ya magenge hayo ya  Wahindu. 

Wahindu wenye misimamo mikali katika jimbo la Tripura kaskazini mashariki mwa India wamekuwa wakiwahujumu Waislamu na kuharibu misikiti minne kwa sababu ya kulipia kisasi kutokana na kile wanachodai ni kusumbuliwa Wahindu katika nchi jirani ya Bangladesh.

Kufuatia hali hiyo, wakuu wa eneo hilo wamepiga marufuku mijimuiko ya watu zaidi ya wanne na kuonya kuhusu jumbe chochezi katika mitandao ya kijamii.

Jimbo la Tripura lina mpaka wa kilimota 850 na nchi ya Bangladesh ambayo wakazi wake wengi ni Waislamu. Hivi karibuni nchini Bangladesh watu waliokuwa na hasira walivamia hekalu la Wahindu ambapo watu saba walipoteza maisha katika ghasia hizo.

Machafuko hayo yaliibuka baada ya kuenea klipu iliyooneysha Msahafu ukiwe umewekwa katika goti la kijimungu cha Kihindu jambo ambalo liliwakasirisha Waislamu na kuibua ghasia katika wilaya 12 nchini Bangladesh.

/4008805/

captcha